kama
ajali ulikuja
Moyoni
mwangu ukatua
Nikashindwa
jizuia
Pendo
langu nikakupa
Nikadhani
nimepata
Mwandani
wa kunifaa
Kumbe
we ni shubiri
Uchungu
wanipatia
Bila
huruma waumiza
Ndani
ya pendo hilo
Kwako
mtumwa nikawa
Kwangu
Ukawa mtwana
Mkali
usiye huruma
Siku
dakika pia saa
Bila
kuchoka bila kusita
Kila
huduma nilikupatia
Kwa
sasa nimechoka
Njia
yangu ninaenda
Asante
kwa kunitesa
Moyo
wangu kuuchoma
Mbali
na mboni yako
Mbali
na mateso yako
Sasa
huru nimepata
Hitaji
la moyo wangu
Moyo
wangu utacheka
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni