Jumatano, 20 Februari 2019

Kibamia Meniponza by Beautus Kusaga

*Kibamia meniponza*

Nilipika mboga yangu
Kisha nikatia nazi
Cheza na nyanya mafungu
Kuuonesha ujuzi
Kusudi isiwe chungu
Viungo vikawa Shazi
*Kibamia meniponza*
*Bora nisingekuweka*

Chumvi nikairamba
Ili radha kuionja
kisha nikajigamba
Bila sura kuikunja
Na kichwa  kikanivimba
Nikajiona ni ninja
*Kibamia meniponza*
*Bora nisingekuweka*

Mboga ilipokaribia
Nikatoa mfuniko
Nikatia kibamia
Kiivie hukohuko
Yalokuja kutokea
Kweli ni mfadhaiko
*Kibamia meniponza*
*Bora nisingekuweka*

Kikaiharibu mboga
Sababu ya kuteleza
Nikaingiwa uoga
Jicho likawa kengeza
Nabaki kupiga soga
Ili muda kupoteza
*Kibamia meniponza*
*Bora nisingekuw eka*

Sifa mapishi ufundi
Chakula kiwe kitam
Uliza nani hapendi?
Chakula kitie ham
Usijetia mtindi
Kwenye nyama ni haram
*Kibamia meniponza*
*Bora nisingekuw eka*

✍🏿 Beatus kusaga
    Reporter

      Kasuku
  0719368158