Ilikua mchana Siku yenye furaha
Siku ya kukutana Na wangu mwanana
Mpenzi Tuliyependana na kushibana
Moyo wake ulikua nyumba ninayoipenda
Siku ya sherehe, sherehe ya kuagana
Alipendeza usoni kwangu
Alipendeza moyoni kwangu
Kila aliyemuona macho kama kingu
Minono ilikika sifa kwa mpenzi wangu
Kweli Alipendeza kwa wengine na kwangu
Kwa mwendo wa madaha mikononi alinijia
Nami nikampokea kwa tabasamu na furaha
Kwa busu mdomoni ndivyo hunisalimia
Muziki kifunguliwa kwa pamoja kuucheza
Muda ukawadia, muda wa kuagana
Siku zikapita, miezi ikapita, miaka ikapita
Kila kona nilitafuta, kila mtu niliuliza
Bila mafanikio sura yake sikuona tena
Moyo kudhohofika, pendo lake kulikosa
Alikua furaha yangu sikumwona tena
Nilisikia yoko huku kwenda kuli patupu
Nilisikia ameenda huku, nako nilikuta tupu
Moyo wangu ulipondeka kukosa wake upendo
Kumbukumbu iliyobakia ilinitesa kama upupu
Ikiťokea kumuona, ikitokea kumsalimia
Mwambie nampenda, moyoni mwangu ni tupu
Aje kunitoa huu upweke, uumao kama jipu.
Poet: Onesmo Ndile
Language: kiswahili
Year: 2013
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni