Jumatatu, 10 Oktoba 2016

Nasi tuliwapokea

Asubuhi na mapema, Upepo mkali ulivuma
Kando kando ya bahari, Likatokea kubwa dubwana
Tukiwa na nyingi tahamaki, Ghafla liliachama
Wakatoka viumbe wa ajabu, Weupe kama theluji
    Nasi tukawapokea

walikuja na nyingi zawadi, Nguo shanga na mawaridi
Iyo yote kutulaghai, nia yao si zawadi
Ndani tukawakaribisha, kwa machungwa na machenza
Taratibu tuliwazoea, lugha yao kujifunza
Elimu mpya walitupatia,  hiyo yote kutuzuga
    Nasi tukawapokea

Taratibu walianza badilika, kila kitu kutupora
Mateso kutupatia, bila huruma wala msamaha
Vilivyo thamani kichukua, visi thamani kutuachia
Wadogo kushughulisha, wazee kutuulia
    Nasi tuliwapokea

Harakati tulianzisha, ukombozi kuutafuta
Wakubwa kwa wadogo, pamoja twashirikiana
Kwa ngumi hata kwa panga, kwa visu hata kwa kamba
Tulipogana tukapigana, kwa jasho na damu kutoka
    Nasi tukawaondoa 

Miaka miezi kupita, furaha kuturudia
Amani kutawala, matunda kujivunia
Wazee kwa vijana, wote twafurahia
Upendo kutawala, heshima twasimania
    Nasi twafurahia

alasiri na mapema, anga lilojema
Dubwana likaangu, kutoka angani juani
Ubavuni pakafunguka, viumbe wakatokea
Kwa chakula na kwa fedha, viongozi kuwateka
Kumbukumbu yasahaulika, nyumbani kuwaingiza
    Nasi tumewapokea.

Author: Onesmo Ndile
Language: Kiswahili
Year: 2016

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni