Ijumaa, 7 Oktoba 2016

Nimezama



Uwepo wake hupendeza machoni
Mguso wake husisimua moyoni
Tabasamu kama maua hujaa usoni
Upweke unitoa na roho kunisuuza
      Nimezama kwako ewe kasuku

Uzuri wa macho yake hakuna mfano
Nyororo sauti yake ni wimbo moyoni
Uimbwa kwa maringo na madaha kitandani
Msisimuko akilini kwa papaso kifuani
     Nimezama kwako ewe kasuku

Yake ngozi laini hunikosha moyoni
Mabusu kedekede yote kwangu mwilini
Roho yangu iteke nibebe nisi pweke
Usijenipiga mateke na kuniacha mpweke
     Nimezama kwa ewe kasuku

Nimezama kwako malkia ni kwako hiyo pete
Mola atujalie milele tupendane
Milele uwe wangu milele niwe wako
Tushikane tugandane mithili ya kupe
Nakuomba tulia, mimi ni wako peke.
      Nimezama kwako ewe kasuku

Author: Onesmo Ndile
Language: Kiswahili
Year: 2016
 

Maoni 2 :

  1. Big up broo unanikumbusha shairi
    Pendo tamu kama hili halina mfano wake
    Halina hali yake mithili duniani liko Pweke
    ladha kushinda asali huko kufanana kwake....

    JibuFuta